Usijipe Stress Kwa Kukosa Jambo fulani Katika Maisha,Mwisho Wa Usiku Utakufa Tu

Jana nikiwa katika mishe mishe ndani ya Daslamu,kwanza nilipita sehemu nikaona watu bwana wana makazi mazuri sana,yani unapata hamu hata ya kuwahi kurudi home,nyumba kali,garden kali na swimming pool ya kiushikaji.

Jamani kuna watu wanaishi kwenye makazi mazuri na kuna sisi tumejaaliwa kujistiri tupate pakulala na kujihifadhi

Nikiwa njiani ndani ya jiji la Daslamu,nakutana na ndinga kali barabarani,jamani kuna watu wana drive ndinga na wengine tuna usafiri wa kutoka point moja kwenda nyingine

Unajua nini expert wangu? Iko hivi mwisho wa siku tutakufa,kwahiyo take it ize,yani usiwaze kivile,hatupo duniani milele kwamba ukose raha mbona mimi sipo kama wale au similiki mali kama wale

Kifo kiwe liwazo kwako kwamba hayo yote hayatadumu milele,kwahiyo haina haja ya kukosa raha na furaha,mwisho wa siku hapa duniani tunapita tu

Umekosa makazi ya ndoto yako,just chill usikonde

Umekosa ndinga ya ndoto yako,just chill usikonde

Umemkosa umpendaye kwa dhati,just chill usikonde,coz ipo siku ungekufa wewe au yeye

Kwa kila jambo ambalo limekuwa hamu yako kubwa tambua kwamba one day,huu ulimwengu utaisha na maisha halisi yataanza huko akhera,kikubwa tengeneza mazingira ili upate neema za huko akhera

Ni hayo tu!

Post Reply